viwango duniani vya gesi chafu na joto ya hewa vinaongezeka mwaka baada ya mwaka zaidi ya viwango kabla ya viwanda. © Creative Commons
Sayari yetu inakuwa na joto. Joto kiasi fulani kinatarajiwa, kwa sababu ya jua kuwa kubwa polepole na mabadiliko madogo kwa mzunguko wa dunia. Hata hivyo, athari kama hizi zinaweza kutabiriwa na haziwezi kufafanua joto la kasi tulili nalo sasa. Kiwango hiki cha joto kimepanda sana viwanda vya kibinadamu na usafiri umeendelea. Inaingiana na utabiri mwingine, uliotabiriwa na mwanasayansi Mswidi miaka 150 iliyopita, kwamba ongezeko la gesi nyinginezo ingesababisha hewa kunata joto la jua zaidi. Ongezeko la viwango vya joto vya kushangaza vya gesi chafu, ambayo gesi aina ya cabon dioxide na Methene ni nyingi zaidi.
Kwa hali ya hewa pia? 6
Miaka kumi na miwili ya kujiweka kando katika barafu ya Briksdal Norway, ambayo ilifunika barafu mwongo tu mbeleni © Mateusz Kurzik/Oleg Kozlov/Shutterstock
Ongezeko la joto la dunia lina athari mbili kuu. Athari ya polepole zaidi ni kuyeyuka kwa barafu ukingoni mwa dunia. Barafu katika Antaktika na kisiwa kikubwa zaidi duniani inayeyuka na kutiririka haraka. Inamwaga barafu inayofunika ardhi kuyeyuka baharini mwishowe kuongeza viwango vya maji baharini duniani,kwa pengine kama vile mita moja karne hii. Athari za haraka ni mabadiliko katika hali ya hewa , inayohusishwa na mabadiliko katika joto baharani na katika mitindo ya hali ya hewa inayoathiriwa na joto la baharini. Mvuke zaidi wa maji unapanda hewani kutoka bahari joto zaidi, na mitindo ya hali ya hewa inayobadilika inazipa sehemu nyingine mvua na dhoruba kuliko kawaida. Kwa utofauti, sehemu nyingine zinapokea muda mrefu wa hali kame na ukosefu wa maji yaliyohifadhiwa.
Nini hutokea hali ya hewa inapobadilika
Mafuriko katika Thailand © Atikan Pornchaprasit/Shutterstock
Idadi ya binadamu imekuwa kubwa kwa sababu ya maendeleo ya kilimo wakati wa milenia kadhaa ya hali nzuri ya hali ya hewa. Hata hivyo, ongezeko la viwango vya joto vya kisasa duniani vinatishia binadamu na mazingira katika njia nne: mafuriko, moto, njaa na magonjwa. Mafuriko yanakuwa mabaya zaidi kupitia kuongezeka kwa maji baharini katika nyanda za chini na mvua kubwa anayoosha machanga kwingineko. Muda mrefu wa hali kame inaleta uwezekano wa mimea kukauka , na halafu kuchomeka kwenye moto wa mwituni. Ukame na mafuriko vinaathiri mimea kama chakula cha binadamu na wanyama wengine , kwa hivyo kusababisha njaa inayoweza kuwa mbaya zaidi na ukosefu wa maji ya kunywa. . Athari hizi pia huweka mimea na wanyama hatarini kupata magonjwa ya kitropiki , inayosambaa kuelekea ukingoni mwa dunia katika hali ya hewa mpya ya joto zaidi.
Mioto ya mwituni katika Marekani © ARM/Shutterstock
Viwango vya hewa chafu hupanda na ongezeko la uchomaji wa mafuta asili. ikiwemo makaa ya mawe, mafuta na gesi. Hata kama tutasitisha ochomaji wa mafuta haya asili, ongezeko la polepole la joto la kisasa litachukua miongo mingi kubadilisha. Hata hatari kubwa zaidi ni kwamba ongezeko la viwango vya joto vifikie viwango hatari zaidi ambapo ni vigumu kubadilisha. Hii italeta wasiwasi nyingi sana ya uharibifu wa misitu mikubwa ya tropiki. Iwapo ardhi ya miti itapotezwa kwa moto wa mwituni na mchanga kwa kiangazi, wenyeji lazima wahame. Watu zaidi watakuwa wakimbizi iwapo ongezeko la maji baharini litasukuma dhoruba kusababisha mafuriko katika miji ya pwani. Kuleta huku kwa hali ya wakimbizi kutahatarisha kuhusika kabisa kwa kimataifa kutoka kwa sulihisho za mabadiliko ya hali ya hewa, uhifadhi wa mazingira na kuishi kwetu?
Tunaweza kufanya nini?
Usambasaji wa nishati mpya manyumbani katika Ulaya na Afrika © Hecke61/MrNovel/Shutterstock
Kuna sulihisho za kimazingira kusaidia bahari, mchanga na mimea kukunyonya kaboni zaidi. Kupanda miti kwa wingi zaidi polepole inazalisha mchanga mpya, vile vile kutoa nafasi za kuhifadhi kaboni kwa mbao katika majengo. Njia za kurejesha unyevu wa mchanga kupitia kurejesha mfumo wa ikolojia, haswa katika chemichemi, misitu mipya na kilimo kinachojizalisha upya, inaweza kusaidia sana. Kuna pia suluhisho zilizohandisiwa. Umeme unaozalishwa kutoka kwa jua na upepo unaweza kuchukua nafasi ya mafuta asili katika kutumika manyumbani, viwandani na usafiri, bora tu tunaweza kuwa na njia za kuhufadhi umeme wa kutosha kutumika wakati tulivu wa usiku. Nchi za kaskazini zinahitaji kukubali mitindo endelevu ya kimaisha, na kusaidia nchi za kusini kufanya mabadiliko haya kwa sababu tunatumia sayari moja . Chochote tufanyacho, tunahitaji kukifanya haraka, kabla ya kufikia uharibifu mkubwa sana..