Ujuzi wa kitamaduni wa watu wa kabila la Inuit ulisaidia kusuluhisha maajabu ya safari ya Franklin ya Aktiki iliyomsababishia kifo © WikiCommons
Uongozi ni jinsi jamii ya binadamu inasimami shughuli zake. Si uongozi wa kutoka juu hadi chini tu. Isipokuwa kwenye udikteta, uongozi unahitaji uungwaji mkono mkubwa, unaongozwa na ujuzikulingana na sayansi na/au uzoefu. 'Ëlimu ya kitamaduni' hujijenga kupitia kuangalia kwa muda mrefu kwa mazingira
Maisha ya ndege wa baharini huhatarishwa kupitia uchafuzi, mabadiliko ya hali ya hewa, uvuvi kupita kiasi na uvuvi usiokusudiwa © Marina Rosales Benites de Franco
IUCN ina mchakato wa kufafanua hali ya viumbe unaokubalika duniani, kulingana na ukubwa wa idadi na kiwango cha kupungua. Iwapo hakuna ushahidi thabiti wa kupungua unaotegemea data nzuri, kiumbe kitakuwa cha 'wasiwasi mdogo" ilhali viumbe vyenye idadi iliyokomaa vikipungua kwa nusu haraka ikilingalishwa na maisha yake (kwa kawaida kwa miongo miwili kwa ndege) ni 'kuhatarishwa". Mbinu zikipatikana za kugeuza sababu za kupungua , idadi ya vyote isipokuwa viumbe vikubwa zaidi inaweza kuongezeka haraka mara dufu tena na inaweza kuongezeka zaidi tena. Njia mbili zimepatikana na walio mamlakani kugeuza kupungua katika idadi ya viumbe: Adhabu na thawabu.
Kulinda na kuadhibu
Uchunguzi wa hapo awali wa DNA ulihitaji damu, lakini sasa unahitaji sampuli ndogo © Anatrack Ltd
IUCN pia ina vikundi vya sehemu zinazolindwa, vikitofautiana kutoka kwa ardhi ambako shughuli nyingi za kibinadamu zinaruhusiwa hadi sehemu ambako kufikia kumezuiliwa. Kulinda viumbe pia kunatofautiana kwa nguvu, kutoka kwa kunakotumika tu wakati wa kuzaana hadi kuharamishwa mauaji bila kubagua; Maslahi ya 'haki za wanyama' hata inatamani kupiga marufuku ufugaji wowote wa wanyama. Sheria za kulinda zinafaulu iwapo zina uungwaji mkono wa umma na uvunjaji sheria unagunduliwa kwa urahisi, kwa mfano na uchunguzi wa DNA. Ulinzi haufanikiwi sana kama viumbe vinasababisha uharibifu mkubwa kwa jamii mashinani, haswa iwapo uvunjaji sheria unafichika kwa urahisi. Vikwazo vya kibabe na adhabu, ambazo hazizuii wavunja sheria iwapo hatari ni ya kiwango cha chini, inaweza kubagua jamii za mashinani.
Dhawabu na urejesho
Uthibitisho wa mimea mwitu na FairWild initiative © Traditional Medicinals Inc
Pale ambapo wanyama wanasababisha shida, kuruhusu uthibiti fulani kunaleta uungwaji mkono wa wenyeji. Kudumisha na kurejesha mifumo ya ikolojia kunahitaji juhudi za wenyeji kwa muda mrefu. Sheria haziwezi kulazimisha juhudi zinazohitajika na vikwazo kuhusu usimamizi vinaweza kuzuia juhudi hii. Hata hivyo, iwapo viumbe mwitu vina thamani, na vinatumiwa vizuri kwa muda mrefu, 'kuafikia mahitaji na matarajio ya vizazi vya sasa na vijavyo', jamii zitavihifadhi isipokuwa kama kuweka ua na ukulima kunalipa vizuri zaidi. Kwa kuhifadhi viumbe viletavyo shida zaidi, thawabu hufanya kazi zaidi kuliko kuombwa. Kupata nyama na kuuza haki za uwindaji zenye thamani inaweza kuwa thawabu yenye nguvu zaidi , vile vile utazamaji wa wanyama ambapo utalii unaleta thamani mashinani bila kudhuru mfumo wa ikolojia. Thawabu nyinginezo za uhifadhi ni malipo kutoka kwa serikali kwa usimamizi na tuzo za utendakazi bora. Ni vizuri pia kutumia bidhaa asili zenye vyeti vinavyoonyesha kuwa matumizi yake kwa muda mrefu ni mazuri. Makubaliano ya kimataifa makubwa zaidi ya hivi karibuni ya uhifadhi wa mazingira, Mkataba Kuhusu Utofauti wa Kibaolojia, unataja matumi ya muda mrefu mara tano zaidi kuliko unavyotaja ulinzi.
Uongozi unaoweza kuzoea
Uongozi mzuri unahitaji kuzoea mabadiliko katika hali na ushahidi. Kwa mfano, kiumbe katika wingi kutumiwa kwa muda mrefu kinaweza kuwa nadra na kinahitaji kulindwa, lakini hadi tu uwingi wake umerejeshwa, ili kurejelea kwa manufaa kutoka kwa matumizi ya muda mrefu kunatoa motisha ya uhifadhi wa mfumo wake wa ikolojia tena. Watu kwingineko huja wapinge matumizi mapya iwapo kiumbe kimekuwa nembo ya ulinzi au utalii, au pesa zinapatikana kwa kufikia matarajio kupitia uzalishaji wa kinyumbani. Kunaweza kuwa na mwito wa vizuizi na kufuatilia kwa kina ambayo wenyeji hawawezi kutimiza bila kusaidiwa. Hata hivyo wale wanaothamini na kuthibiti ardhi wanakoishi kwa kawaida wana uwezo wa hakika kuhifadhi 'mazingira yao', iwapo wataongozwa kwa makini, kuliko wale wanaotamani kulinda wanyamapori wa watu wengine. Uongozi mzuri unahusisha kutengeneza sheria zinzoweza kuendeleza uhifadhi kupitia utendakazi mzuri na kuwawezesha wenyeji kunufaika tena kwa muda mrefu.Bara la Ulaya limepitisha makubaliano yanayosisitiza kanuni hizi; Makubaliano ya Uhifadhi wa Viumbe vya Kuhamahama yamefanya kazi katika kuweka viumbe ma ndege wanaowala kupitia mipango ya makubaliano ya pamoja.