Manufaa na tishio kwa mfumo wa Ikolojia.
Mavuno kutoka baharini © Anatrack Ltd
Kwa nini tunathamini mazingira? Ni kwa sababu unategemea mazingira kwa riziki yako,kama vile watu wengi mashinani katika nchi kadhaa? Unapenda kuchuma matunda ya mwituni na kuvu au samaki au kuwinda katika njia tofauti? Katika nchi nyingine, chakula hutoka sana sana madukani, lakini kwa jumla zaidi ya thuluthi moja ya watu pia wana tamaduni kubwa za kutafuta chakula kutoka kwa mazingira. Pengine unapenda kutazama wanyama, pengine kujituliza na kufanya mazoezi? Kama ni hivyo, unatumia tunachoita manufaa na huduma za kitamaduni za mfumo wa ikolojia. Moto wa mwituni, mafuriko na mkurupuko wa wadudu kwa mimie au manyumbani huwa ni matokea ya mfumo wa ikolojia ambapo uthibiti wa huduma umeharibiwa. Kila mtu anategemea mchakato wa mfumo wa ikolojia unaounga mkono hewa inayoweza kupumuliwa, maji safi na hali ya hewa inayokubalika.
Athari za binadamu kwa mfumo wa ikolojia
Viwanda vinaweza kuchafua hewa, mchanga na maji © Hramovnick/Shutterstock
Tunaporekebisha mazingira kwa manufaa yetu kunaweza kuwa na athari mbaya. Katika sehemu zenye rotuba, nyasi, misitu na hata chemichemi zinaweza kugeuzwa kuwa mashamba ya ukulima, na upanzi wa mimiea aina moja inayoondoa mimea muhimu kwa viumbe asili vingi na mwishowe matokeo ya upungufu wa rotuba mchangani. Katika sehemu zisizostahili ukulima mkubwa, wanyama wa nyumbani wanaweza kuchukua nafasi ya wanyama wa mwituni, na mabadiliko zaidi ya uondoaji wa wanyama wanaokula wanyama wengine na ongezeko la shinikizo la malisho kwa mimea. Katika sehemu za rotuba ndogo zaidi au sehemu zisizoweza kufikiwa, kama vile sehemu zilizojaa barafu, chemichemi na jangwa, kuongeza matumizi ya kujifurahisha kwa sehemu hizi kunaweza kuwa na athari mbaya, kukibaki na nyika ndogo ya kweli. Hata bila athari za kimakusudi na wenyeji na jamii za kibinadamu zinazozuru, utupaji wa plastiki duniani, na vichafuzi vya hewa na maji, hufika hata sehemu za ndani kabisa, usisahau mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni. Shida zingine huenea kutoka kwa usambasaji wa magonjwa bila kujua na uzinduzi wa viumbe vinavyoonyesha kustawi zaidi kuliko vilivyoko tayari. Shida hizi zote zinaweza kupunguza huduma ambayo mfumo wa ikolojia hutoa kwa binadamu na kwa viumbe vingine ambavyo tunatumia pamoja ulimwengu.
Kuthibiti athari za binadamu kwa mfumo wa ikolojia.
Shida zinapotokea, jamii za mashinani huzigundua na wakati mwingine kuzitatua kupitia urejesho wa gharama nafuu. ujuzi kadhaa unahitajika kuthibiti huduma za mfumo wa ikoloji, ikiwemo juhudi za vitendo za wakulima mashinani, watunza misitu, wavuvi, wawindaji, wanaopenda wanyama pori, wavunaji mwituni na watunza bustani, wakisaidiwa na wanasayansi na mara kwa mara kufadhiliwa na serekali. Utajiri asili mkubwa wa mfumo wa ikolojia unaweza kurejeshwa kwa kiwango fulani, ukipewa muda wa kutosha na hali zinazofaa. Vitu vingine kama vile mimea na viumbe vodogo na wanyama wengineo wadogo, wanaweza kurejeshwa haraka katika hali nyingi; hata hivyo, misitu iliyokomaa huchukua miongo kuzalishwa tena, na mchanga wa juu wenye rotuba unaweza kuchukua karne nyingi kurutubisha. Kwa kuongoza na kuwezesha kazi kama hii, wanasayansi na serikali wanahitaji kuelewa jinsi ya kuhimiza na kusaidia jitihada za wenyeji. Wenyeji wanaweza kuhimizwa kuchangia katika uhifadhi na kushirikisha wengine katika maarifa yao wakikubaliwa matumizi madogo na yanayosaidia ya raslimali iliyoimarishwa.